Monday, March 25, 2019

Waziri Lugola aagiza Polisi kushugulikia chama cha siasa kitakachofanya mikutano ya hadhara

SHARE
Na. Thabit Hamidu, Zanzibar

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza jeshi la polisi nchini kushughulikia chama chochote cha siasa ambacho kitakachokiuka taratibu  ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara.

Alisema kuna baadhi ya vyama vya siasa nchini vimekuwa vikikiuka taratibu kwa kufanya mikutano ya hadhara jambo ambalo limeshapigwa marufuku na serikali.

“Naliagiza jeshi la polisi kupitia kwa kamshna kuwashika wale wote ambao wanakiuka taratibu wanafanya mikutano ya hadhara na kutishia amani na utulivu wa ulipo nchini.

Hayo aliyabanisha leo wakati akisikiliza kero za wananchi mbali visiwani Zanzibar katika kiwanja cha Komba wapya Wilaya ya Mjini Zanzibar.

Alisema huu si wakati wa Vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhala badala yake wakite katika kushughulia maendeleo ya nchi.

Alisema kufanya mikutano ya siasa na shughuli mbalimbali za siasa ni kurejesha nyuma maendeleo ya nchi.

"Mimi nataka niwambie kuwa huu si wakati wakutambulishana vyama na kufanya mambo ya siasa wanachotakiwa mambo ambayo yatawaingizia kipato na kuunga jitihada za marais wetu” alisema Waiziri.

"Nataka kuwambia kuwa hatutaangalia nafasi yqa mtu, wingi wa madevu aliokuwa nao sisi tutamshughulikia endapo akikuuka taratibu na kutishia amni ya Nchi”aliongeza kufafanua.

Katika hatua nyingine waziri Lugola alikemea vitendo vya udhalilishaji vinavyofanya na baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi na baadhi ya watendaji wa serikai.

“Tunataarifa kuwa kuna baadhi ya afisa wa jeshi la polisi hufanya vitendo vya udhalilishaji na mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa kazi zao tukimbaini tutamshughulikia”alisema Waziri.

Aidha waziri aliwaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kufichua wahalifu katika mitaa yao.

Mapema akimkaribisha Waziri Naibu waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Yusuf Masauni alisema hali ya amani na utulivu katika mkoa wa Mjini magharib jambo ambalo linachanguia ukuwaji wa Uchumi.

Alisema kuna baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikijaribu kuvyunja amani kwa kuandaa mikutano kinyume na sheria lakini Jeshi la polisi litahakikisha linadhibiti mikutano hiyo ili kuiendeleza kuna baadhi ya Vyama vya siasa vimekuwa vinaanza kuharibu amani kwa kufanya mikutano yao kinyume amani iliopo.

Aidha Akizungumzia suala la Udhalilishaji wa kijinsia Masauni alisema bado tatizo la udhalilishaji limekuwa tatizo kutokana na baadhi ya Wananchi kutokubali kutoa ushahidi wakati kesi zikisikilizwa sehemu husika.

Alisema wakati umefika kwa wananchi kuthamini juhudi za serikali katika kupambana na tatizo la Udhalilishaji wa wanawake na watoto ili kutokomeza tatizo hilo Nchini.

Katika mkutano huo Waziri huyo alipata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Mjini Magharib  Unguja na kuahidi kuzitatua haraka iwezekanavyo.

Mkuno huo ni muendelezo wa ziara zake Nchini katika kusikiliza malalamiko kwa wananchi yanayohusiana na Wizara yake.
SHARE

Author: verified_user

0 Comments: