Monday, April 29, 2019

Kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdad ajitokeza katika kanda ya video baada ya miaka 5

SHARE
Kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdad

Kundi la Islamic State limetoa kanda ya video ya mtu linayedai kuwa kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi, ambaye ameapa kulipiza kisasi kwa kupoteza himaya yake.
Hajaonekana tangu 2014 , wakati alipodai kuunda taifa linalofuata sheria ya kiislamu nchini Syria na Iraq.
Katika kanda yake mpya, Baghdad alikiri kupoteza eneo la Baghuz ambalo ndio ngome ya mwisho ya kundi hilo katika eneo hilo.

Haijulikani ni lini kanda hiyo ya Video ilirekodiwa . IS inasema kuwa ilichukuliwa mnamo mwezi Aprili .
Kanda hiyo ya video ilichapishwa katika tovuti ya kundi hilo ya al-Furqan.
Msemaji wa wizara ya kigeni nchini Marekani anasema kuwa kanda hiyo itachunguzwa na wachanganuzi ili kubaini inakotoka, akiongezea kwamba muungano wa majeshi ya Marekani utaendelea kuhakikisha kuwa kiongozi yeyote wa kundi hilo aliyesalia anakamatwa ili kuchukuliwa hatua kali.

Anasemaje?

Baghdadi anasema kuwa shambulio la Jumapili ya Pasaka nchini Sri Lanka lilikuwa shambulio la kulipiza kisasi baada ya kundi hilo kupoteza mji wa Baghuz nchini Iraq.
Pia amesema kuwa ameahidiwa kuungwa mkono na wapiganaji wa Burkina Faso na Mali na mazungumzo kuhusu maandamano ya Sudan na Algeria akidai kwamba Vita vya Jihad ndio suluhu dhidi maadui zao.
Mataifa yote mawili yamepoteza viongozi wao wa muda mrefu mwezi huu.
Hatahivyo picha ya Baghdad inapotea mwisho wa kanda hiyo huku sauti yake akikzungumzia shambulio la Sri lanka inachezwa badala yake- ikimaanisha kwamba kipande hicho cha sauti kilirekodiwa baada ya kanda ya video kuchukuliwa.

Baghdadi akihutubia wafuasi wake mjini Mosul, 2014
 Abu Bakr al-Baghdadi, ambaye hajawahi kuonekana katika kamera tangu 2014 ameapa kulipiza kisasi. 

Baghdadi - ambaye ni raia wa Iraq kwa jina Ibrahim Awwad Ibrahim al-Badri - sauti yake ilisikika mara ya mwisho katika kanda iliorekodiwa mwezi Agosti.
Wakati huo, alionekana akitafuta kuvutia gumzo wakati ambapo kundi lake lilikuwa likipoteza maeneo lililonyakuwa , kulingana na mwandishi wa BBC mashariki ya kati Martin Patience.
Lakini kanda hiyo ya video ya dakika 18 inaangazia hasara ya kundi hilo moja kwa moja.
Vita vya kudhibiti mji wa Baghuz vimekwisha , anasema, akiongezea : Kutakuwa na mengi baada ya vita hivyo.
Pia ameongezea kwamba kundi hilo linapigana vita vya kiakili.

Je uongozi wa taifa la Kiislamu ulipotea wapi?

Katika kilele chake, IS ilitawala eneo la zaidi ya kilomita 88,000 mraba hadi karibu na mpaka wa Iraq na Syria .
Lakini 2016 kundi hilo lilinza kusalimu amri.
Mwaka uliofuatia lilipoteza ngome yake kuu Mosul nchini Iraq, wakimnyima Baghdad na wafuasi wake mji ambao walikuwa wameunda taifa la kiislamu.

Ramani nne zinaonysha jinsi eneo hilo lililokiuwa likimilikiwa na IS lilivyopungua
Ramani nne zinaonysha jinsi eneo hilo lililokiuwa likimilikiwa na IS lilivyopungua
Mnamo mwezi Oktoba kundi hilo lilifurushwa kutoka katika mji wa Raqqa nchini Syria.
Liliendelea kupoteza himaya yake mwaka 2018 hatua iliofanya kundi hilo kurudi nyuma hadi Baghuz.
Hatahivyo wapiganaji wa Kikurdi SDF walitangaza kwamba wameukomboa mji huo, na kutangaza kumalizika kwa uongozi wa Kiislamu wa miaka mitano mnamo mwezi Machi 2019.
Je Abu Bakr al-Baghdadi ni nani?
Alizaliwa 1971 katika eneo la Samarra nchini Iraq.
Akiwa angali mtoto alidaiwa kupenda sama kusoma Quran na kufuata sheria za kidini, akiwalaumu ndugu zake wasiofutwa vizuri dini ya Kiislamu.
Lakini ilikuwa wakati ambapo alikuwa anafuzu kupata Stashahada ya somo la Quran katika chuo kikuu cha Saddam Husein , ndio wakati alijihusisha na msimamo mkali wa kundi hilo.
Mwisho wa mwaka 2000 alikuwa ameanzisha kundi linalofuata sunna na aliendelea hadi kushirikishwa na kundi la al-qaeda nchini Iraq ambapo kundi la Islamic state lilibuniwa.
Tangu 2014 amesalia mkimya kwa muda mrefu huku kukiwa na uvumi wa kifo chake ambao haujathibitishwa.


SHARE

Author: verified_user

0 Comments: