Tuesday, April 30, 2019

Bobi Wine arudishwa rumande Uganda

SHARE
Bobi Wine

Kumekuwa na hisia kali kufuatia taarifa kwamba mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amerudishwa rumande mpaka Mei 2 siku ya Alhamisi wiki hii.
Ameshtakiwa kwa kushiriki katika maandamano ya 'haramu' mnamo mwaka jana ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii maarufu Uganda kama OTT.
Alionekana akitembea huku akiwa amefungwa pingu mikononi kabla ya kuabiri basi la magereza kuelekea katika gereza kuu la Luzira mjini Kampala.

Haya yanafanyika siku chache baada ya kuwa katika kifungo cha nyumbani.
Ameshtakiwa kwa kuandaa maandamano ya umma kinyume na sheria, na alizuiwa siku ya Jumatatu katika kituo cha polisi cha Naggalama kwa mujibu wa taarifa ya polisi.
Msemaji wa idara hiyo Fred Enanga amesema Bobi Wine aliongoza maandamano hayo mwaka jana pasi kwanza kuomba ruhusa kutoka kwa polisi.
"Anazuiwa na polisi na uchunguzi unaendelea," ameliamba shirika la habari la AFP.
Kampeni mpya imeanzishwa katika mitandao ya kutaka Bobi Wine aachiliwe huru huku baadhi wakizungumzia hatua hiyo kama ya kutia wasiwasi.

Ujumbe wa Twitter wa @CossyWyne: Fighting for equal rights and justice #FreeBobiWine

Ujumbe wa Twitter wa @kaysafi1: May we learn to be as strong &resilient as you've been so far Bobi Wine. May we speak on the things that matter &emulate you.You make not only I but many like myself proud of being youths. You give us purpose. We love you! Stay strong. #FreeBobiwine ✊🏾✊🏾

Mashirika ya kutetea haki za binaadamu likiwemo la Marekani, Tom Lantos Human Rights Commission, na shirika linaloshinikiza uongozi wenye maadili na demokrasia kwa wote - Vanguard Africa, yameshutumu hatua hiyo ya serikali ya Uganda.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, mashirika hayo yametaka serikali iheshimu uhuru wa kujieleza na kushinikiza kuachiwa kwa mwansiasa huyo wa upinzani.

 Aliyekuwa waziri mkuu wa New Zealand Helen Clark amejiunga katika kutoa ujumbe huo wa kutaka Bobi Wine aachiwe kwa kuitisha mshikamano wa kitaifa katika kulinda maisha na afya ya mwanasiasa huyo wa Uganda.
Ujumbe wa Twitter wa @HelenClarkNZ: Very distressing to see #Uganda 🇺🇬 opposition MP & popular musician #BobiWine detained again. Last year in detention he was beaten & tortured. International solidarity is vital to protect Bobi's health & life #FreeBobiWine @commonwealthsec @VanguardAfrica
Bobi Wine aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika kile ambacho polisi walisema ilikwa ni hatua ya kumzuwia mwanasiasa huyo wa upinzani kufanya mikutano iliyo kinyume cha sheria.
"Hizo zilikuwa ni hatua zilizochukuliwa chini ya sera ya kuzuwia ili kulinda sheria na utulivu wa umma. Wakati bado anatishia kufanya mikutano kinyume cha sheria ,maafisa wetu wa ujasusi watatusaidia kumpata na tutaweza kuona ni nini kitakachofuatia. Hata hivyo hadi sasa tutaendelea pale majeshi yetu kwasababu hili limekuwa ni suala la usalama wa taifa ," amesema Msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga.
Saa kadhaa awali , Bobi Wine alikuwa ametangaza mpango wa kufanya maandamano ya umma kote nchini kupinga hatua ya polisi kuendelea kuweka vikwazo dhidi ya tamasha zake za mziki na ukatili dhidi ya wanasiasa wa upinzani.

Bobi Wine ni nani?

Bobi Wine "Bobi amepata ufuasi kwa nemba yake ya 'nguvu za watu',"


Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, hna anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.
Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.
Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).
Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia.
"Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki...Ninataka siasa zitulete pamoja... jinsi muziki ufanyavyo."
Mchambuzi wa kisiasa Nicholas Sengoba anasema "Bobi amepata ufuasi kwa nemba yake ya 'nguvu za watu',"Bobi amepata ufuasi kwa nemba yake ya 'nguvu za watu', na ananuia kushinikiza na kupanga liwe vuguvugu".

Mchambuzi wa kisiasa Robert Kirunda anasema mvuto wa Wines unatokana na kuwepo 'pengo la uongozi' Uganda.
"Kuna vijana wengi Uganda ambao hawana haja ya kujua vita vya kihistoria vilivyoiingiza NRM uongozini, au ukaidi wa upinzani mkuu. Wengi wanataka ajira na wanahisi uchumi hauwasaidi."
Kirunda anasema Wine 'anapigia upatu sana'. "Anaweza kushinikiza watu pakubwa, lakini bado hajapata nguvu kama alizonazo Besigye katika upinzani".

SHARE

Author: verified_user

0 Comments: