Mkazi wa Kijiji cha Nyantorotolo Kata ya Nyankumbu Halmashauri ya Mji wa
Geita, Patrick Andre (41) anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Geita kwa
tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kufikia wa miaka 7, ambaye ni mwanafunzi
wa darasa la pili.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli
Mwabulambo amesema kwa sasa jina la mtoto huyo wanalihifadhi, lakini
alikuwa akisoma Shule ya Msingi Nyankumbu, ambapo ameeleza mwanamume
huyo alifanya kitendo hicho majira ya saa tano usiku siku ya mkesha wa
Pasaka.
Aidha Kamanda Mponjoli amesema mtu pekee ambaye aligundua mtoto
kufanyiwa vitendo hivyo vya kinyama ni mama mzazi wa mtoto huyo, ambaye
pia alibainisha kulihifadhi jina lake.
0 Comments:
Post a Comment