Rais John Magufuli ameendelea kusistiza kuwa maendeleo ya nchi hayana chama ingawa anaamini maendeleo ya uhakika yanaletwa na kiongozi kutoka CCM.
Ameeeleza hayo akiwa katika ziara yake mkoani Mbeya ambapo leo anatarajiwa kufungua kuaweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Katumba – Mbambo – Tukuyu na ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Kikusya – Matema.
"Maendeleo haya chama, sisi wote tunahitaji maendeleo, lakini nina uhakika maendeleo ya kweli na kiongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi ambaye atawajibika kuwatumikia Watanzania wote, tumechelewa,
Ameendelea kwa kusema, "Tukitengeneza barabara hata CHADEMA watapita, nashangaa hapa hakuna hata kituo cha mabasi, yaani niwe mbunge wa hapa nishindwe kusema eneo hili liwe kituo cha mabasi watu wafanye biashara".
0 Comments:
Post a Comment