Serikali imesema kuwa hakuna dawa yoyote ambayo kitaalamu imethibitishwa na imepewa kibali kwa ajili ya matumizi ya kukuza maumbile. Wale ambao wanatoa taarifa hizi bila ya udhibitisho wanatakiwa wachukuliwe hatua.
Hayo yamesemwa leo bungeni na Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi ambapo ameeleza kumekuwa na taarifa nyingi za dawa zinazoweza kukuza maumbile kitu ambacho sio sahihi.
"TFDA haijawahi kupokea taarifa za madhara kuhusiana na kucha za kubandika kutokana na kukosekana kwa takwimu hizo, serikali haioni sababu ya kufunga saluni zote wala kuwachukulia hatua wanaotoa huduma hii".Waziri Mwinyi (kwa niaba ya waziri wa Afya).
Ameendelea kwa kusema "Katika mwaka wa fedha 2017/18 TFDA ilipokea kutoka kwa watumiaji na watendaji wa afya taarifa 238 za madhara yaliyohisiwa kusababishwa na matumizi ya dawa ambapo tathmini zilionyesha kuwa ni salama na zinafaa kuendelea kutumika".
0 Comments:
Post a Comment