Tuesday, April 23, 2019

Tutafanya kila tuwezalo kuilinda na kuitetea Quds

SHARE


Amir wa Kuwait Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah amesisitiza msimamo wa nchi yake katika kuinga mkono na kuitetea Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah amebainisha kwamba, Palestina ndiyo kadhia kuu ya Ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, nchi yake ya Kuwait itafanya kila iwezalo katika kuiunga mkono na kuitetea Palestina.

Amir wa Kuwait amesema hayo katika mazungumzo yake na Nabil Abu  Rudeinah, Naibu Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kueleza kwamba, Kuwait inaunga mkono kwa dhati haki za kisheria za taifa la Palestina.

Amesema, Kuwait itaendelea kulitetea na kuliunga mkono taifa la Palestina na kwamba, nchi yake inatambua kwamba, kadhia ya Palestina ni jambo la awali linalopaswa kupewa kipaumbele katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa upande wake, Nabil Abuu Rudeinah, Naibu Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameisifu na kuipongeza misimamo ya Kuwait ya kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, harakati za kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na nchi za Kiarabu zimeongezeka zaidi miongoni mwa baadhi ya nchi za Kiarabu, baada ya Benjamin Netanyahu kufanya safari nchini Oman Oktoba mwaka jana, hatua ambayo ilipelekea Oman iandamwe kwa ukosoaji mkubwa kieneo na kimataifa.
SHARE

Author: verified_user

0 Comments: