Monday, April 29, 2019

Watu 2,175,500 wangeathiriwa na kimbunga Kenneth

SHARE
Na Ahmad Mmow, Lindi.
Watu 2,175,500 wangeathiriwa na madhara ya kimbunga Kenneth iwapo kingetokea katika baadhi ya maeneo ya nchi kama ilivyotabiriwa.
Hayo yameelezwa leo na mkurugenzi wa  idara ya maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matemwe wakati wa kikao cha tathimini ya ununuzi wa korosho msimu wa 2018/2019 na maandalizi ya ununuzi wa ufuta msimu wa 2019/2020 katika mkoa wa Lindi.  Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi.

Matemwe alisema iwapo kimbunga hicho kingetokea hapa nchini katika baadhi ya maeneo kama ilivyotabiriwa,watu 2,175,500 wangeathirika.Ikiwamo uharibifu wa mali na baadhi yao kufariki.

Alisema tathimini iliyotolewa na wataalamu inaonesha kingetokea hapa nchini halmshauri 12 zilizopo katika maeneo yaliyotabiriwa kufikiwa  zingeathirika.


" Kwa kasi ya kimbunga Kenneth nikwamba ambao wangekiona wasingepona. Kwahiyo wananchi waendelee kuwa na tabia ya kutii maelekezo ya viongozi wanapotahàdharishwa ili waweze kujiokoa,"  alisema Kanali Matemwe.

Matemwe aliishukuru serikali ya mkoa wa Lindi kwa kufanya maandalizi ya kukabiliana na madhara ya kimbunga hicho iwapo kingetokea. Hata hivyo alitoa wito wa kuendelea kutolewa elimu kwa wananchi kuhusu maafa.

Alisema uimara wa kamati za maafa za mikoa unategemea uimara wa kamati za maafa za ngazi ya chini yake (wilaya hadi vijiji na mitaa) na mtu mmoja mmoja. Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa wakutoa elimu kwa wananchi.
SHARE

Author: verified_user

0 Comments: