Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:
INARUHUSIWA KUWASILIANA MARA KWA MARA NA MCHUMBA WAKO? KWA SIMU AMA BARUA AMA E-MAIL?
JIBU:
Sifa zote
njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola wa
walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla
Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu
'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Ama
kuhusu kuwasiliana baina ya mvulana aliyeposa na posa yake kukubaliwa
na msichana na walii wake basi hakuna tatizo lolote ikiwa mawasiliano
yao ni katika mipaka ya kishariy'ah na mbele ya Mahaarim.
Wanachuoni
wanaonelea mawasiliano baina ya wachumba kwa simu au kwa njia nyingine
za faragha zozote zile hayaruhusiwi. Yote ni katika kuepusha fitnah na
Shaytwaan kuingia baina yao kabla ya ndoa.
Mara
nyingi mawasiliano ya karibu kabla ya ndoa, yameleta uharibifu mkubwa
na madhara katika jamii na kusababisha posa nyingi kuharibika na hata
watu kutumbukia katika zinaa.
Mbali
na mawasiliano hayo mvulana anaweza kwenda nyumbani kwa mchumba wake
bora tu wasikae faragha wao peke yao katika mazungumzo. Inabidi awe
pamoja nao Mahaarim wa msichana. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakai faragha mwanamume na mwanamke ila wa tatu wao ni Shaytwaan. Na hakika Shaytwaan hutembea katika mwili wa mwana Aadam kama itembeavyo damu”.
Hii
ni kuwa bado nyinyi hamjakuwa mume na mke, na mmoja kati yenu anaweza
kuvunja ndoa hiyo baada ya kuwa mmekubaliana hapo awali. Mwanamume
anaweza kusema basi hataki tena harusi au mwanamke vilevile kuamua kuwa
hakuna tena harusi, na baya zaidi ni uwezekano wa kutokea maovu katika
kipindi hicho.
Ile
desturi ya wachumba kuwa wanakwenda pamoja katika mabustani, sinema au
kusafiri kabla ya kuoana si desturi ya Kiislamu, japo kuna nchi nyingi
za Waislamu wanafanya hivyo.
0 Comments:
Post a Comment