Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:
Asalaam alykum warahmatulahie wabarakatuh naomba Allaah swt
awalipe malipo wazuri kuhusu kazi mnayoifanya awaweke katika pepo ya
juu firdaus ameen Allaahuma ameen mimi. Nilikiwa ninaswahi. Mimi niko na
mchumba na tunataka kuowana lakini bado myaka michache nimalize shule
na haiwezekani tukafanya harusi kwa sasa lakini nafanya subra mpaka
nimalize shule ndo tuowane je kwa hivi sio haram??
JIBU
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza
kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la
Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama
ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya
kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kumtaja Allaah, na
andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na
ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama
inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada
inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza
au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na
hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.
Shukrani
zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuolewa ukiwa katika masomo. Ndoa
katika Uislamu ni maafikiano na ahadi ambazo wanachukua mume na mke
katika njia ya halali. Ikiwa tayari umechumbiwa na mume na tayari
mumeagana kuoana baada ya masomo inabidi wewe na yeye muepukane kabisa
ili msije mkaingia katika madhambi.
Haifai
Kiislamu watu walioposana kukutana faragha wala kuzungumza hata kwa
simu ili lisije likatokea jambo ambalo halifai. Inabidi kila mmoja
asubiri na aepukane na vishawishi vyote ambavyo vinaweza kuwakaribisha
na zinaa. Ikiwa mnaona ya kwamba hamuwezi kuvumilia basi inabidi muoane
ili muepukane na madhambi.
Tufahamu
kuwa hakuna jambo lisilowezekana, wapo wasichana wengi walioolewa na
wakaendelea na masomo bila matatizo. Ikiwa hamuwezi kusubiri na
kujizuilia itabidi muoane na lau mtaweza kusubiri bila kuingia katika
maasiya basi itabdi mfanye subira hadi mmalize malengo yenu ya masomo
ndio muoane.
Tunamuomba Allaah Awape subira katika hilo, Aamiyn.
0 Comments:
Post a Comment