Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:
Assalamualeikum
Bismillahirrahmanirrahim
Alhamdulillah,
mimi ni mwanamke wa miaka 21, nna kazi yangu na nipo masomoni kusomea
hiyo kazi. Nina mchumba wangu hayupo hapa, yupo ulaya anatafuta maisha
na ameshakuja kuleta wazee wake kwa wazee wangu lakini bado
haijakubalika sababu wamesema wanataka miaka minne kwa ajili ya
matayarisho ya kazi na kimaisha ya huyu mwanamme...jee inafaa mimi kua
naongea nae? Na pia kupeana ushauri wa maisha yanavokwenda? Je inafaa?
Wabillahi tawfiq
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani
zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuongea na mchumba wako ambaye
amekataliwa na wazee wako. Mazungumzo baina ya mwanamme na mwanamke ni
njia moja ya kukaribia zinaa, hiyo ni kuwa Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katujulisha kila kiungo cha
mwanaadamu kinazini, mdomo ukiwa ndani ya tangazo hilo. Na Allaah Aliyetukuka Ametunasihi kuwa tusikaribie zinaa (al-Israa’ [17]: 32).
Na
kulingana na swali lako wazee wako wamekataa posa mpaka baada ya miaka
minne wakati ambao mchumba wako atakuwa amestakiri kimaisha. Kwa hiyo,
wewe na yeye hamna hata hayo mahusiano ya uchumba. Kwa ajili hiyo, ni
bora msiwe mkizungumza kungojea wakati atakapokuja tena na kuposa na
kukubaliwa. Hata ikiwa amekubaliwa ni bora kuchukua tahadhari kubwa
katika mazungumzo.
Kukubaliwa
posa kwa mwanamme si kibali cha kuzungumza mnayotaka kwani hajakuwa
mumeo. Kile kinachokubaliwa baada ya posa ikibidi ni yale mawasiliano ya
muhimu yenye kuhusiana na masuala ya muhimu ambayo yasiyoingiliana na
mapenzi na hisia ili Shaytwaan asiingie kati yenu.
0 Comments:
Post a Comment