MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi, unatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu wiki ijayo, kutoka Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Mwanasheria wa Familia ya Marehemu Dk. Mengi, Michael Ngalo ametoa kauli hiyo nyumbani kwa marehemu leo tarehe 3 Mei 2019 wakati akitoa ratiba ya shughuli za mazishi ya Dk. Mengi ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa nchini.
Wakili Ngalo amesema, Dk. Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2019, ataagwa siku ya Jumanne tarehe 7 Mei 2019 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Na kwamba, baada ya mwili wa Dk. Mengi kuagwa, siku ya Jumatano tarehe 8 Mei 2019 utasafirishwa kuelekea Machame wilayani Moshi, Kilimanjaro.
Akitangaza ratiba hiyo nyumbani kwake Kinondoni leo, Wakili Ngalo amesema, ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamisi katika Kanisa la KKKT, Kisereni na kisha kuzikwa.
0 Comments:
Post a Comment