Friday, May 3, 2019

TEF yatoa rai kwa serikali

SHARE
Sanduku la kura
JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limeishauri serikali kuunda chombo maalumu, kitakachofanya kazi ya kutoa mwongozo kwa wanahabari na vyombo vya dola, juu ya kuripoti masuala ya uchaguzi. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).
Wito huo umetolewa leo tarehe 3 Mei 2019 na Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile katika maazimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayohitimishwa jijini Dodoma.
Balile ameeleza kuwa, katika kipindi hiki ambacho Taifa linajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, ni vyema chombo hicho kikaundwa ili kuwaongoza wanahabari na vyombo vya dola.
“Tueshuhudia mara kadhaa unapokaribia uchaguzi, urafiki kati ya wanasiasa na vyombo vya habari hugeuka kuwa urafiki wa mashaka, ukizingatia sheria za uchaguzi za Tanzania na Zanzibar bado zimeiweka tasnia ya habari katika tanuru la mtanziko,” amesema Balile.
Balile ameeleza kuwa, inapofika kipindi cha uchaguzi wanahabari hukabiliwa na changamoto mbalimbali, kwa kuwa urafiki wao na baadhi ya wanasiasa hugeuka kuwa wa mashaka.
Amesema, kama chombo hicho hakitaundwa, usalama na uhuru wa wanahabari utakuwa mashakani.
“Mwaka huu tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani kutakuwa na uchaguzi mkuu, tunaamini kupitia maazimisho haya na kwa kuwa kidunia kauli mbiu inazungumzia uchaguzi na demokrasia,” amesema Balile na kuongeza.
“ Basi dola na vyombo vya habari, tuunde chombo kitakachotoa muongozo kwa vyombo vya habari na dola wakati wa uchaguzi kwani bila kufanya hivyo, tunaamini uhuru na usalama wa habari utakuwa mashakani.”
SHARE

Author: verified_user

0 Comments: