Friday, May 3, 2019

RATIBA KAMILI MAZISHI YA DK MENGI -VIDEO

SHARE


Marehemu Dk Reginald Abraham Mengi enzi za uhai wake.
Mchana huu Mwanasheria wa familia ya marehemu bilionea, Dk Reginald Abraham Mengi, Michael Ngalo ametoa ratiba ya mazishi ya mwenyekiti huyo mtendaji wa IPP.

Ngalo amesema kuwa mwili wa marehemu Mengi utawasilia saa 8:00 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates. Amesema baada ya hapo, mwili huo utakwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, siku hiyo ya Jumatatu. Amesema Jumanne, mwili huo utapelekwa kwenye Viwanja vya Karimjee, Posta jijini Dar kwa ajili ya kuagwa na wakazi wa Dar na viunga vyake. Baada ya kuagwa Karimjee, mwili huo utapelekwa nyumbani kwa Mengi, Ada-Estate, Kinondoni jijini Dar hadi kesho yake, Siku ya Jumatano, mwili wake utapelekwa uwanja wa ndege tayari kwa kusafirishwa kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kisha kijijini Nkuu, Machame kwa mazishi yatakayofanyika Alhamisi ijayo.
SHARE

Author: verified_user

0 Comments: