FIKRA kwamba, Rais John Magufuli angeongeza mishahara kwa wafanyakazi wa sekta ya umma leo, zimetoka patupu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ jijini Mbeya leo tarehe 1 Mei 2019, Rais Magufuli amesema, serikali inakabiliwa na changamoto ya gharama za uendeshaji ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi, deni la taifa pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Hata hivyo
amesema, ahadi yake ya kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma pamoja
na kutatua changamoto zao iko pale pale na kwamba, kwa sasa amejikita
katika kuimarisha uchumi wa nchi ili hata watakapoongezewa mishahara
fedha zao ziwe na thamani.
Rais Magufuli
amesema, gharama za kuendesha serikali ni kubwa na kwamba kiasi cha
fedha kinachobakia ni kidogo, hivyo fedha hizo ni bora zipelekwe katika
miradi ya maendeleo ili kukuza uchumi wa nchi.
“Gharama
za kuendesha serikali bado ni kubwa, tunatumia takribani Sh. 580 Bil,
kulipa mishahara kila mwezi, kwa bahati nzuri siku hizi tunalipa tangu
tarehe 19 suala ambalo lilikuwa halipo, najua hili tungelipa hata tarehe
2 msingeshangilia,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;
“Lakini
pamoja na kwamba tunalipa kila mwezi, bado hicho kiasi kilichobaki
tunatakiwa kulipa madeni ya mkopo. Tunatakiwa pia tushughulikie miradi
ya maendeleo hivyo mnaweza kuona wenyewe tunatumia kiasi gani, na
kinachobaki tumekuwa tukijiuliza tukipeleke wapi.”
Kwenye
maadhimisho hayo Rais Magufuli amesema, “hapo ndipo tumekuwa pia
tukijiuliza kama mkulima mwenye mbegu anavyojiuliza wakati wa njaa,
atumie kwa chakula au azitunze ili msimu wa mvua azipande zimletee
chakula.”
Ametoa
mfano huo huo kwa wafanyabiashara kwamba, anavyojiuliza atumie mtaji
wake kutatua shida zake au atafute shughuli nyingine za kumuongezea
vipato na sisi tumekuwa tukijiuliza.
“Tuliona
ni busara kutumia kiasi kidogo ili kilichobaki tukiweke katika miradi
ya maendeleo ili kuchochea uchumi, na kukuza uchumi kwa kasi zaidi,”
amesema.
Rais
Magufuli amesisitiza kuwa, ahadi yake ya kuongeza mishahara kwa
watumishi wa umma kabla ya uongozi wake wa awamu ya kwanza kuisha iko
palepale, na kuwataka watumishi kuwa na subira.
“Naomba
muamini kwamba subira yavuta kheri, muda wangu bado haujaisha, ungeweza
kusema napandisha sh. 5000 kesho bidhaa zingepanda, ni lazima tujenge
uchumi imara. Ndugu zangu kupanga ni kuchagua, tungesema hakuna kuajiri
hizi tunagawana posho, ninachotaka kuwaeleza ahadi yangu bado haijaisha,
muda wangu wa utawala bado haujaisha,” amesema Rais Magufuli na
kuongeza;
“Na
kwa muelekeo unavyoenda kwa mambo yanavyoenda na mimi naamini
yatafanikiwa kadiri ya uchumi wetu unavyoenda kwa sababu uchumi wetu
bado unakua kwa silimia 7.
“Tanzania
ni nchi miongoni mwa nchi tano Afrika ambao uchumi wake unakuwa kwa
kasi, na kwa uchapakazi unaofanywa na wakulima, na wafanyabaishara
tunaelekea pazuri, nimeamua niwaeleze ukweli na ukweli utabaki palepale,
kwa hiyo ndugu zangu mvumilie, sikutaka kuwapaka uji kwa kusema
nimepandisha.”
Aidha,
Rais Magufuli amesema tangu serikali yake iiingie madarakani imetatua
changamoto za watumishi wa umma ikiwemo kutoa nyongeza ya mshahara yenye
thamani zaidi ya 72 bilioni, kupandisha madaraja watumishi 118989
ambapo kiasi cha Sh. Bilioni 29 zimetumika, pia amesema kwa mwaka ujao
wa fedha wa 2019/20 serikali itapandisha madaraja watumishi 193,169.
Pia,
amesema serikali imelipa deni ililokuwa inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya
jamii kiasi cha sh. Trilioni 1.5, imeajiri watumishi 42,735 ambao
mishahara yapo ugharimu Sh. 25.8 bilioni kila mwezi, pia amesema
itaajiri watumishi 45,000 mwaka ujao wa fedha.
0 Comments:
Post a Comment