Friday, May 3, 2019

Rais Magufuli awaonya wanafunzi wa vyuo

SHARE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka vijana kusoma kwa bidii na kuachana na masuala ya mapenzi kabla ya wakati.

Ameeeleza hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Teknolojia Mbeya (MUST) ambapo amewataka waalimu kuwa wakali kusimami nidhamu.

"Wakati naingia hapa nimeona binti amekumbatiana na kijana mmoja, Mimi kama huyo binti angekuwa binti yangu ningeshuka nikawachape vibao wote. Sidhani kama kuna mzazi anamtuma wanaye kukumbatiwa na jamaa hata mahari hajatoa,

Ameendelea kwa kusema, "Wanangu someni, msisahau mlikotoka, wengi mmetoka kwenye familia maskini kama mimi, someni, maana ninyi ndiyo marais wa baadaye, mawaziri, maprofesa na fanyeni kile wazazi wenu walichowatuma," amesema JPM.

SHARE

Author: verified_user

0 Comments: