Comments Off on Mabasi ya mwendokasi yasitisha safari zake, barabara zafungwa
Kampuni ya UDA-RT imeutaarifu umma kuwa huduma za mabasi
yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, imesitisha huduma zake kati ya
Kimara – Kivukoni, Kimara – Gerezani, Morroco – Kivukoni na Morroco –
Gerezani kuanzia saa 10: 30 alfajiri leo Jumatatu Mei 13, 2019.
Hatua hiyo ni kufuatia kujaa maji katika eneo la Jangwani.
Huduma zinazotolewa sasa ni kati ya Kimara – Mbezi, Kimara – Magomeni Mapipa, Kimara – Morroco, Gerezani – Muhimbili, Kivukoni – Muhimbili na Gerezani – Kivukoni.
Aidha ufuatiliaji unaendelea kuona hali ya maji katika eneo husika, ambapo kama maji yakipungua huduma zitarejea katika hali ya kawaida.
Wameomba radhi kwa usumbufu kutokana na kusitishwa kwa safari hizo.
Hata hivyo barabara ya Kinondoni kwenda Magomeni imefungwa, Magari yote hayapiti kutokana na bonde la Mkwajuni kujaa maji.
0 Comments:
Post a Comment