Thursday, May 2, 2019

Rais Magufuli aeleza alivyoguswa na kifo cha Dkt. Reginald Mengi

SHARE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametuma Salamu za pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi.

Kifo cha Dkt. Mengi kimetokea usiku wa kuamkia leo Alhamis Mei 2, 2019 huko Dubai katika falme za Kiarabu. Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika;

"Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo katika kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara," ameeleza Rais Magufuli.
 Rais John Magufuli akipeana mkono wa watoto wa Dkt.Regnald Mengi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Regnald Mengi kinachoitwa “I can,I must,I will”,hafla iliyofanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es salaam, Julai 2,2018.
SHARE

Author: verified_user

0 Comments: