Unafahamu nini kuhusu suala la kumlaza mwanao? Maana Mapokeo tuliyo
yapokea enzi na enzi ni kuwa ukitaka mtoto wako alale bila kushtuka basi
alalie tumbo. Bado watu wengi wanaendelea kufanya hivyo hata sasa hivi
unaposoma makala haya.
Je madaktari wanasemaje kuhusu suala hili?
Sayansi inashauri kuwa ni hatari kumlaza mtoto kwa tumbo. Visa kadhaa
vya watoto kupoteza maisha vimehusishwa na watoto kulalia tumbo.
Kuanzia mwaka 1992 Madaktari wa watoto nchini Marekani walipendekeza
kuwa watoto wachanga walale chali ( walalie Mgongo) ili kuepuka vifo vya
ghafla vya watoto. Kifo cha ghafla hutokea pale ambapo mtoto mchanga
anakutwa amefariki akiwa usingizini.
Tangu pendekezo hilo la madaktari idadi ya vifo vya ghafla vya watoto
imepungua zaidi ya nusu ya vifo vyote vya watoto vinavyotokea wakiwa
usingizini.
Ni vizuri kuhakikisha kuwa kila mtu anayekusaidia kulea mtoto anajua jinsi ya kumlaza mtoto chali.
Muhimu
Hata hivyo kuna baadhi ya watoto unaweza kushauriwa na daktari iwapo mwanao usimlaze chali na alalie tumbo.
0 Comments:
Post a Comment