Kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia hivi sasa, kila kitu ninaweza kufanyika pasipo hata watu kuonana kwa macho.
Hiyo pia hutokea hata kwa wapenzi ambao
wanaweza kuwasiliana moja kwa moja bila kuonana, ikiwa ni pamoja na
kutumiana picha, sauti na video kwa lengo la kufurahishana. Mara
nyingine picha hizo zinaweza kuwa si nzuri sana kutumwa mtandaoni kwa
kuwa ni za faragha.
Akilielezea hilo katika kipindi cha
Mjadala cha EATV, mtaalam wa masuala ya kimtandao, Maxence Melo amesema
kuwa kitu kinachosababisha ujumbe wowote kuvuja mtandandaoni pasipo
wahusika kusambaza ni kuingiliwa kwa mawasiliano ya kimtandao.
"Si rahisi kwa ujumbe wowote wa
faragha kuvuja mtandaoni pasipo watu waliotumiana kuhusika au kuwepo kwa
pengo linaloruhusu kwa sababu unapokuwa unatuma ujumbe wowote
mtandaoni, unaweza ukaingiliwa na mtu wa kati ambao ni wadukuzi",
amesema.
"Lakini pili, kifaa cha mhusika
kinaweza kikawa ni sababu pia ya kuvuja kwa sababu watu wengi wanaotumia
hasa simu za android wanapakua 'application' mbalimbali ambazo zingine
zinachukua taarifa za mtumiaji na kutuma kwa watu wengine bila ya
mtumiaji kujua", ameongeza.
Mtaalam huyo amesisitiza kuwa si salama
kwa wapenzi kutumiana picha mtandaoni hata kama wanaaminiana na
kusisitiza kuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria za mtandao, kipengele cha
14 kwa mtu kuchukua video ya faragha na kuitengeneza kwa lengo lolote na
adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 7 au faini isiyopungua
milioni 20.
0 Comments:
Post a Comment