Wednesday, May 15, 2019

WhatsApp: Fahamu namna ya kuwa salama unapotumia mitandao ya kijamii

WhatsApp: Fahamu namna ya kuwa salama unapotumia mitandao ya kijamii


whatsapp logo

Taarifa kwamba "WhatsApp inaweza kudukuliwa" sio jambo ambalo mtumiaji yoyote wa mtandao huo wa kijamii anataka kusikia wala kuona katika kichwa cha habari.
Alafu kuongezea kwamba "Wadukuzi walifanikiwa kuweka mfumo wa uangalizi" na kitengo cha habari cha kampuni hiyo wana kibarua kikubwa mikononi mwao.
WhatsApp linasema akaunti kadhaa zililengwa na " mdukuzi mkuu wa mitandao".

Lakini iwapo kauli hii imekutia wasiwasi, haya ni baadhi ya mambo unayostahili kufanya kuhakikisha mawasiliano yako yapo salama.

Udukuzi huo uligunduliwa kwanza mapema mwezi huu.
Wakati huo Facebook, inayomiliki mtandao wa WhatsApp, iliwaambia maafisa wa usalama kwamba lilikuwa : "pengo katika mawasiliano ya sauti ya WhatsApp VOIP [voice over internet protocol] iliyoruhusu udukuzi kupitia vifurushi vya mfumo wa SRTCP [secure real-time transport protocol] vilivyotumwa kwa nambari ya simu ya mlengwa."

Hata kama simu haikushikwa, mfumo huo wa udukuzi uliidhinishwa kutokana na pengo hilo katika mawasiliano ya sauti ambao hauna usalama wa kutosha.
Simu pengine ilikatika na haionekani kwenye orodha ya waliopiga simu katika simu yenyewe, kwasababu wadukuzi walikuwa tayari wameidhibiti.

messaging logos


kulinda usalama wa taarifa zako whatsapp fanya yafuatayo!!!
  1. nenda katika whatsapp setting
  2. bofya account .
  3. bofya tena two step verification
  4. bofya tena enable
  5. weka PIN/namba za siri
  6. bofya tena change email adress ,weka email
  7. bofya tena confirm email
  8. mwisho bofya done. utakuwa umemaliza!!!


Usihifadhi taarifa zako kwenye anga la mtandao

cyber attack
Licha ya kwamba mawasiliano yanalindwa katika WhatsApp, epuka kuhifadhi taarifa zako kwenye anga la mtandao kama Google Drive au iCloud, hapo kuna tatizo.
Anga hilo la mtandao halina usalama kwahivyo mtu yoyote anaweza kuingia na kuyafikia mawaslinao yako yote.


Iwapo unajali faragha, basi hilo ni jambo ambalo unapaswa kufikiria kuacha kulifanya.
Huenda ukapata ujumbe kwamba hifadhi mawasiliano yako - lakini iwapo unataka kulibadili hilo hivi sasa nenda kwenye eneo la kuhifadhi chati zako yaani Chat Backup, katika eneo la mpangilio wa simu yako - settings.

Programu saidizi za kuimarisha ulinzi

cyber attack

Kuna programu saidizi za kuimarisha ulinzi, uthibitisho wa mara mbili (2FA) kabla kuingia kwenye mtandao huo ambao ni njia nzuri ya kuweka data yako salama.
Ni kama wingu la ziada la usalama kuhakikisha watu wanaojaribu kuingia katika akaunti ya mtandao ni watu asili wanaosemakuwa ni wao.

Kwanza, mteja ataingiza jina lake na nywila. Baada ya hapo watahitajika kutoa alama za vidole, au sauti yao au nambari maalum zitakazotumwa na programu hiyo kwenye simu yako ambazo utatumia kufungua na kuingia kwenye akaunti ya Whatsapp na nyinginezo za kijamii.
Unaweza kulibadili hilo pia kwenye upande wa mpangilio wako wa simu.


Monday, May 13, 2019

Mabasi ya mwendokasi yasitisha safari zake, barabara zafungwa

Mabasi ya mwendokasi yasitisha safari zake, barabara zafungwa



1 min ago Comments Off on Mabasi ya mwendokasi yasitisha safari zake, barabara zafungwa
Kampuni ya UDA-RT imeutaarifu umma kuwa huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, imesitisha huduma zake kati ya Kimara – Kivukoni, Kimara – Gerezani, Morroco – Kivukoni na Morroco – Gerezani kuanzia saa 10: 30 alfajiri leo Jumatatu Mei 13, 2019.
Hatua hiyo ni kufuatia kujaa maji katika eneo la Jangwani.
Huduma zinazotolewa sasa ni kati ya Kimara – Mbezi, Kimara – Magomeni Mapipa, Kimara – Morroco, Gerezani – Muhimbili, Kivukoni – Muhimbili na Gerezani – Kivukoni.
Aidha ufuatiliaji unaendelea kuona hali ya maji katika eneo husika, ambapo kama maji yakipungua huduma zitarejea katika hali ya kawaida.
Wameomba radhi kwa usumbufu kutokana na kusitishwa kwa safari hizo.
Hata hivyo barabara ya Kinondoni kwenda Magomeni imefungwa, Magari yote hayapiti kutokana na bonde la Mkwajuni kujaa maji.
Nyakati Tatu Muhimu Za Kufanya 'Ibaadah Zisikupite Katika Ramadhwaan

Nyakati Tatu Muhimu Za Kufanya 'Ibaadah Zisikupite Katika Ramadhwaan

Image result for RAMADHAN



Japokuwa nyakati zote za siku katika mwezi wa Ramadhwaan ni tukufu, ila nyakati hizi tatu ni muhimu mno za kutekeleza ‘ibaadah kutokana na fadhila zake adhimu.   Mwenye kupenda kuchuma thawabu nyingi asizikose khaswa katika mwezi huu mtukufu Wa Ramadhwaan ambao ni mwezi wenye malipo maradufu.


1-Wakati wa mwanzo:  Baina ya Alfajiri na jua kuchomoza:

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaamrisha kumsabbih katika wakati huu kama Anavyosema:

وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ﴿٣٩﴾
Na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. [Qaaf: 39]
 وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا ۖ  
Na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua, na kabla kukuchwa kwake.    [Twaahaa: 130].

Pia, usimulizi uliothibiti kutoka katika Swahiyh Muslim (564/1) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba walikuwa wakibakia macho wakati huo hadi jua kuchomoza kwani ni wakati mja anapogaiwa rizki yake, na ni wakati wenye kheri nyingi. Pia ni wakati unaosababisha kuwa na siha nzuri ya mwili. Kwa ujumla, ni wakati wenye baraka nyingi za kila aina kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba: 

((اللهم بارك لأمتي في بكورها))  الترمذي ، أحمد ، أبو داود ، ابن ماجه 
((Ee Allaah, wabarikie Ummah wangu nyakati za asubuhi mapema)) [At-Tirmidhiy, Ahmad, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah na imethibitishwa kuwa ni Hadiyth Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy]

Usimulizi huu umetoka kwa Maswahaba kadhaa ambao wameelezea kwamba: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipotaka kupeleka kikosi au jeshi aliwapeleka mwanzo wa asubuhi." Vile vile wamesimulia kwamba: "Swakhar alikuwa mtu tajiri ambaye alikuwa akipelekea biashara zake mwanzo wa asubuhi na matokeo yake ilikuwa ni kufuzu katika biashara na kupata faida kubwa sana."

Wamesimulia Salafus-Swaalih kwamba Ibn 'Abbaas naye alimkataza mtu kulala nyakati hizo alipomwambia:
   "قُم، أتنام في الساعة التي تقسَّم فيه الأرزاق؟"
"Inuka! Je, unalala katika saa ambayo rizki inagaiwa?"
 
Ibnul-Qayyim (Rahimahu-Allaah) katika 'Zaad Al-Ma'aad' amesema: "Usingizi wa asubuhi unanyima rizki kwani huo ni wakati ambao Muumba anaombwa rizki na wakati wa kugaiwa rizki. Hivyo usingizi unanyima rizki isipokuwa kwa dharura. Usingizi wakati huo pia ni madhara kwa mwili…"  

Faida nyingine kubwa ya kubakia macho ukimdhukuru Allaah wakati huu


عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال: ((مَنْ صَلَّى الْغَدَاةَ فِي جَمَاعَةٍ ثُمَّ قَعَدَ يَذْكُرُ اللَّهَ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ ، ثُمَّ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ ، كَانَتْ لَهُ كَأَجْرِ حَجَّةٍ ، وَعُمْرَةٍ ، تَامَّةٍ ، تَامَّةٍ ، تَامَّةٍ)) رواه الترمذي (586) أخرج الترمذي  صححه الألباني .
Imetoka kwa Anas kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jamaa'ah kisha akakaa anamdhukuru  Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy na kaisahihisha Al-Albaaniy]
Kwa muda wa saa moja na nusu takriban utakuwa umepata thawabu za Hajj na ‘Umrah zikiwa kamilifu. Pindi ukifanya hivyo kila siku kwa mwezi mzima, utakuwa umechuma thawabu za Hajj na ‘Umrah za mwezi mzima. Hizo ni fadhila za siku za kawaida, seuze ukifanya mwezi mtukufu huu wa Ramadhwaan?

Kwa Rahmah ya Allaah (‘Azza wa Jalla) Amejaalia thawabu hizo ziweze kuchumwa tukiwa majumbani mwetu tena kwa wepesi kabisa. Wanaume inawapasa waswali Msikitini kuzipata thawabu hizo kwa kuwa Hadiyth imetaja atakayeswali jamaa’ah. Ama wanawake, wanazipata fadhila hizo hata wakiswali majumbani mwao kama alivyosema Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah) katika Fatwa yake alipoulizwa kuhusu wanawake kama nao watapata fadhila hizo.

Hata hivyo, juu ya kuweko fadhila kama hiyo, tusisahau kuwa haivunji wala haifuti fardh ya kwenda Hajj kwa mwenye uwezo, asije mtu akadhani kufanya hayo kutakuwa kumetengua wajibu wake wa kuhiji au kufanya ‘Umrah.

Tanbihi: Hadiyth hiyo wamekhitilafiana ‘Ulamaa usahihi wake, kuna waliosema ni dhaifu na wengineo wameipa daraja ya Hasan kama Imaam Al-Albaaniy.

Kuna waliosema kuwa inaingia katika mlango wa kumdhukuru Allaah (‘Azza wa Jalla) kwa wingi kama Alivyoamrisha katika Qur-aan khasa katika wakati huo wa kabla kuchomoza jua  [Fataawa Nuwr ‘Alad-Darb lil-‘Uthaymiyn (2/9)] kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿٤١﴾
Enyi walioamini!  Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru.

وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٤٢﴾
Na Msabbihini asubuhi na jioni‏.[Al-Ahzaab 41-42]

Ama Imaam Bin Baaz (Rahimahu Allaah) aliulizwa kuhusu usahihi wa Hadiyth hii akasema: “Hadiyth hii laa baas, kwani inazingatiwa kuwa ni “Hasan lighayrih” na Swalaah hii inapendekezwa baada ya kuchomoza jua na kupanda kwake yaani takriban baada ya robo saa au thuluthi baada ya kuchomoza kwake jua.” [Fataawaa Shaykh Bin Baaz (25/171).

Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) alipoulizwa kuhusu Hadiyth hiyo na fadhila zake kuhusu uhakika wa kuwa atakayetenda atapata thawabu kama za Hajj na ‘Umrah au vipi akajibu: “Kwanza Hadiyth hiyo ina shaka, kwani wengi katika ya ‘Ulamaa wameidhoofisha.  Pili, tukichukuliwa kuwa Hadiyth imethibiti basi thawabu zake hazina kiasi, huenda mtu akatenda ‘amali chache lakini thawabu zake zikawa tele kwa sababu thawabu ni fadhila kutoka kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) Humpa Amtakaye.” [Liqaa Ash-Shahriyy (22/74)]


2- Wakati wa pili: Kabla ya Jua kuzama (Magharibi)

Huu ni wakati ambao bado Muislamu yuko katika Swawm na du'aa yake anayoiomba hairudi:

 قال صلى الله عليه وسلم: ((ثَلاثةٌ لا تُرَدُّ دعوتُهم: الصَّائم حتَّى يُفْطِر، والإمام العادِل، ودعْوة المظْلوم)) وروى الترمذي  بسند حسن
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (([Watu] watatu du'aa zao hazirudi; mwenye Swawm hadi afuturu. Kiongozi muadilifu na mtu aliyedhulumiwa)) [At-Tirmidhiy kwa isnaad nzuri]

Ni fursa kwa Muislamu atumie wakati huo kuomba du'aa wakati huu hasa kwa vile ni wakati ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Amehimiza Atukuzwe kama Anavyosema:

 وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ﴿٥٥﴾
Na omba maghfirah kwa dhambi zako, na sabbih kwa Himidi za Rabb wako jioni na asubuhi. [Ghaafir: 55]

 وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ﴿٣٩﴾
Na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. [Qaaf: 39]
 وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا ۖ  
Na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua, na kabla kukuchwa kwake.    [Twaahaa: 130].



3-Wakati wa tatu: Suhuwr - Kabla ya Alfajiri:

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewaaahidi wenye taqwa wapate kuingia Jannah kwa sababu miongoni mwa sifa zao ni kuomba maghfirah wakati wa suhuwr (kabla ya Alfajiri). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿١٥﴾
Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu. 

آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾
Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani.

كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾
Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha. 

وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿١٨﴾
Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah. [Adh-Dhaariyaat: 15-18]

Kisha wamesifiwa tena kwa sifa kama hiyo pamoja na nyinginezo:

 الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾
Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji mali katika njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri. [Aal-‘Imraan: 17]

Muislamu asiache wakati huo umpite kwani ni wakati muhimu na wenye fadhila na faida kubwa kwa vile Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Huteremka katika thuluthi ya mwisho ya usiku kutoka ‘Arshi Yake na kufika mbingu ya kwanza kuwatakabaliwa waja Wake yale wanayomuomba kama ilivyotajwa katika Hadiyth:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba du’aa Nimuitike? Nani Ananiomba jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

Nani miongoni mwetu asiyemhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kumtakabalia haja zake au kumuondeshea shida zake? Nani asiyekuwa na madhambi ya kuhitaji kughufuriwa? Hivyo usiache wakati huu ukakupita kamwe kufanya ‘ibaadah, ikiwa ni mwezi wa Ramadhwaan au miezi mingineyo.


Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atujaalie tawfiyq ya kudiriki nyakati hizo tatu na kumudhukuru kwa wingi kwa kusoma Qur-aan, kumsabbih, kumhimidi, kumpwekesha na kumtukuza, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).  Na tunamuomba pia Atutakabalie na Atujaalie miongoni mwa watakaoepushwa na moto. Aamiyn 
KIDHI HAJA -Hikma Ya Ruhusa Ya Ukewenza

KIDHI HAJA -Hikma Ya Ruhusa Ya Ukewenza

Image result for NIKAAH

Mume Na Mke


Kuna sababu nyingi za kibinafsi, kimaadili, kiuchumi na kijamii zinazoonesha kuwa wakati mwengine kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilobudi.

Kabla ya kulieleza jambo hili ni vyema tukaelewa nini maana hasa ya ndoa (Nikaah) katika Uislam. Ndoa ni mkataba ('Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislam.

Kwani umuhimu wa ndoa kwa mtazamo wa Uislam ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake katika kujenga na kuendeleza jamii. Kama Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Alivyosema katika kitabu Chake kitukufu cha Qur-aan Suratun-Nuur, Aayah ya 32:
((Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyeezi Mungu Atawatajirisha kwa fadhila Yake. Na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua)) [An-Nuur: 32]
Tafsiri yake ni kwamba:
Na waozesheni wajane miongoni mwenu (waungwana) na walio wema katika watumwa wema (wanaume) na wajakazi wenu.

Pia vile vile Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Suratun-Nisaa, Aayah ya 3:
((… oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu)
Tafsiri:
Oeni walio wazuri miongoni mwa wanawake wawili, watatu na wanne, ikiwa munaogopea uadilifu kwa wanawake hao basi oeni mmoja.

Hii inadhihirisha kuwa tendo la ndoa lina umuhimu mkubwa katika jamii, ambazo zimetubainishia kuwa ndoa ni ngao ya kujikinga na kitendo kichafu cha zinaa.

Mwenyezi Mungu Amehalalisha ndoa na kuitilia mkazo kwa wale wenye uwezo kama tunavyojifunza katika Aayah zifuatazo:
“…na mumehalalishiwa (kwa wanawake) mahari ya hawa muyatafute kwa mali zenu, kwa kuwaoa bila ya kufanya zinaa…” (4:24)

Pia katika surah ya (5:5)
((Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini bila shaka amali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara)) 

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba: 
“Enyi vijana na atakaeweza kati yenu gharama za ndoa (mahari) na aoe”

Pia katika hadithi nyengine amesema:
'Abdullaah bin Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema “Enyi kongamano la vijana na aoe yule alie na uwezo miongoni mwenu, hakika kunainamisha macho (na matamanio) na kuhifadhi tupu (humzuilia mtu na zinaa)na asiyeweza kuoa na afunge, Hakika funga hukata matamanio (Al-Bukhaary na Muslim).

Pia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mmoja wenu atakapomuona mwanamke kisha akamtamani, hana budi kumuendea mkewe kwani ana kile alichonacho huyo mwanamke aliyemtamani” (At-Tirmidhy)

Ndoa ni Sunnah lakini itakuwa wajibu kwa mwenye kuweza na akawa anayo matamanio na anaogopa kutumbukia katika zinaa.

Katika suala la kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilo budi, kwa kuangalia mifano kadhaa kama vile:

a)        Kama mke ni tasa
Mfikirie mwanamme ambae amehakikisha kuwa mkewe ni tasa na bado ana    hamu ya kupata mtoto atakayekuwa mrithi wake. Katika hali hii mwanamme huyu atafanya mojawapo katika haya yafuatayo:

i.        Atakaa na kusononeka kwa kukosa mtoto katika maisha yake yote au
ii.       Atamuacha huyo mwanamke asiyezaa ili aoe mwengine anayezaa au
iii.      Atatembea na mwanamke mwengine nje ya ndoa ili ampatie watoto, japo kisheria si watoto wake au
iv.      Ataendelea kukaa na mkewe kwa mapenzi na furaha kisha aoe mke mwengine atakaemzalia watoto ambao watakuwa wake kisheria.

Utakuta uchaguzi wa kuoa mke wa pili ndio ulio bora kabisa. Wengi katika jamii ya Kiislam wameoa mke wa pili kwa sababu hii.

b)      Kama mke ana maradhi ya kudumu
Mfikirie tena mwanamme ambaye mkewe ana ugonjwa wa kudumu kwa kiasi kwamba hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake kama mke bila ya shaka mwanamme huyu atafanya mojawapo kati ya yafuatayo:

i.        Atajizuia na matamanio yake ya kimwili kwa muda wote wa maisha yake uliobakia au
ii.       Anaweza kumtaliki, mkewe mgonjwa wakati ambapo anahitajia uangalizi, huruma na mapenzi ya hali ya juu kutoka kwake, ili aoe mke mwengine atakayetosheleza mahitaji yake au
iii.       Anaweza kubakia na mkewe mgonjwa na kufanya uzinifu na wanawake wengine nje au
iv.       Ataoa mke wa pili atakayemsaidia kumuhudumia mkewe mgonjwa

Hebu tuzijadili hizi hatua tatu (3) kwa mtazamo wa mafundisho ya Uislam
Hatua ya kwanza: Inakwenda kinyume na umbile la mwanaadamu. Mwenyeezi Mungu Analifahamu fika umbile la mwanaadamu ya haja yake ya kutosheleza matamanio ya jimai na Ameweka utaratibu mzuri wa sheria ya ndoa wa kutosheleza mahitajio haya ya kimaumbile.

Hatua ya pili: Ni kinyume kabisa na ubinaadamu, kumuacha mke kwa sababu amekuwa mgonjwa badala ya kumuhudumia kwa upendo na huruma ni kinyume kabisa na utu. Utaona kuwa hatua ambayo inamuwezesha mume huyu aendelee kumtunza mkewe kwa huruma na wakati huo huo aweze kutosheleza mahitajio yake ya kimaumbile kwa utaratibu mzuri wa heshima ni kuoa mke wa pili

c)       Wanawake wajane
Wajane ni wanawake waliofiwa na waume zao, hakuna jamii isiyokuwa na wajane na idadi yao huongezeka zaidi wakati wa vita ambapo wanaume wengi huuliwa vitani. Je, wanawake hao warudishwe kwa wazazi au walezi wao au kukaa hivyo hivyo bila ya kukidhi matashi yao ya kimaumbile mpaka wazeeke, au waachiwe wawe malaya na kuitokomeza jamii kutokana na matatizo mbali mbali yanayosababishwa na zinaa? Kwa vyovyote vile, njia pekee ya kuwahifadhi wanawake na watoto wao ni hii ruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja hadi wanne, kwa kufuata masharti yaliyowekwa.

d)      Wanawake wakiwa wengi katika jamii
Inatokezea katika jamii nyingi wanawake kuwa wengi zaidi kuliko wanaume. Katika jamii hizi, kama tutaweka sheria ya mume mmoja – mke mmoja kama wanavyodai watetezi wa usawa wa wanawake. Wanawake watakaokosa wa kuwaoa watakwenda wapi? Watafanyaje ili kukidhi matashi yao ya kimaumbile?

Je, kama watazuiliwa mpaka wazeeke huoni hii itawaathiri kimwili, na kifikra na kuwafanya wasiwe watu wenye manufaa katika jamii? Nani watakaotoa hifadhi kwa wanawake hawa kiuchumi na kimaadili? Ilivyo katika maadili ya kibinaadamu, kila mwanamke wa kawaida anahitajia kuwa na mwanamme anayempenda na kumuhurumia, hivyo wanawake hawa watakapokosa waume wa ndoa watafanya kila hila za kuwashawishi wanaume kwa kuwawekea mitego mbali mbali  kama vile kujipitisha mbele yao wakiwa wamejipodoa na kujiremba, kutembea mbele yao uchi, kuzurura kwenye majumba ya sinema n.k. ambayo itawanasa na kuwatumbukiza katika zinaa.

e)      Kuhifadhi jamii na zinaa
Matamanio ya jamii ni katika maumbile na hayaepukiki katika Uislam. Ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake katika kujenga na kuendeleza jamii. Ndoa kwa mtazamo wa Uislam inatarajiwa:
1.     Kuhifadhi jamii na zinaa;
2.     Kuendeleza kizazi cha mwanaadamu kwa   utaratibu mzuri;
3.     Kujenga mapenzi, huruma na ushirikiano katika familia;
4.     Kukuza udugu na ushirikiano katika jamii.

Kwa hivyo kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilo budi kwa mwanaadamu kama tulivyoeleza katika mada yetu hii ya ndoa.


Wa Allaahu A'alam


Du’aa Ya Mada Husika
Ee Mwenyeezi Mungu, hakika mimi nakuomba kheri ya (mke) huyu, na kheri ya maumbile Uliyomuumba nayo, na najilinda Kwako na shari yake na shari ya maumbile Uliyomuumba nayo.
Kumsilimisha Kafiri Na Hukmu Ya Kuoana

Kumsilimisha Kafiri Na Hukmu Ya Kuoana

Image result for NIKAAH 

Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina

SWALI:
 S/A....asanteni sana kwa kuchukuwa time yenu na kulishughulikia swala langu. NATAKA NIJUE HUKMU YA KUSILIMISHA MTU ALAFU AKAKUOWA AU KUMUOWA especially like white people and e.t.c.



JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola   wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tunashukuru kwa swali lako kuhusu mas-ala ya kusilimisha na ikafungamana na ndoa. Tunakukumbusha pia wewe na ndugu zetu wengine wawe ni wenye kuandika Salaam kwa ukamilifu kama tulivyofundishwa na Mtume wetu kipenzi (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akatujulisha thawabu zake. Hivyo kufupisha namna hiyo “S/A” au “A.A.W.W” ni mambo ambayo hatujafundishwa na pia yanatukosesha thawabu zilizotajwa.

Tukirudi kwenye swali, hakuna jambo zuri kama Muislamu kufanya Da‘wah (ulinganiaji) kwa wasiokuwa Waislamu si kwa watu weupe bali kwa binaadamu wote kwa njia moja au nyingine. Jambo hilo lina thawabu kubwa kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Akakuongoza Allaah kwa (kuwa sababu ya kuongoka) mtu mmoja kwako ni bora kwako kuliko ngamia wekundu” (al-Bukhaariy).

Ifahamike kuwa isiwe lengo la kufanya hivyo ni kuoa unayemsilimisha au kuolewa naye. Lengo kubwa ni kufikisha ujumbe na kutaka radhi za Allaah Aliyetukuka.

Hata hivyo ni ubinaadamu kwa mtu kumpenda mwanamme au mwanamke kwa sababu moja au nyingine. Sasa ikiwa umempenda mwenza uliyemsilimisha haifai kucheza naye kwa njia yoyote ile bali inafaa umuoe kisheria ili muweze kuishi kama mume na mke. Hakuna makosa yoyote kisheria kwa kumsilimisha na baadaye wawili hao kuoana lakini kwa uzoefu ulivyo kuna matatizo mengi kwa sababu moja au nyengine. Sababu kuu inayojitokeza ni kuwa mtu husilimu kwa sababu ya kuoa au kuolewa hivyo baada ya kupata matakwa yake hutoka kidogo kidogo katika Dini mpya aliyoingia.
Nadhani katika hili hapana budi ila ni kuwapatia nasaha dada na kaka zetu katika Imani kuhusu mas-ala hayo. Tufahamu kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuhimiza sana tuwe ni wenye kuoa au kuolewa na mwenye Dini na maadili mema. Mtu ambaye amesilimu sasa Dini na maadili yake bado hayajulikani. Kwa hiyo, ni vyema kabla ya kuoana aliyesilimu apelekwe sehemu kwa muda fulani ili apate kufundishwa Dini mpaka imkolee. Katika kipindi hicho inaweza kujulikana ule umadhubuti wake katika Dini. Ikiwa itashindikana basi ni afadhali utafute yule ambaye ni Muislamu tayari.

Kipo kisa kilichotokea Mombasa wakati wa u-Qaadhi wa aliyefariki Shaykh Muhammad Qaasim Mazrui, baada ya Mzungu mmoja kusilimu na kutaka kuoa msichana wa Kiislamu. Wazazi wa msichana wakaenda kwa Shaykh ili kupata ushauri naye akawaambia wamletee huyo mwanamme aliyesilimu. Alipofika ofisini kwake Shaykh alimjaribu kwa kumwambia kuwa msichana hataki tena kuolewa kwa hivyo yeye aweza kuendelea na Uislamu wake. Papo hapo Mzungu huyo alimaka kwa kusema: “Ikiwa msichana amekataa basi mimi sina haja na Uislamu”.

Hivyo, tusiingie katika mtego kama huo kwa kupoteza wasichana wetu au watoto watakaozaliwa katika ndoa hiyo. Tuweni na tahadhari.
Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa

Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa

Image result for NIKAAH

Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:

INARUHUSIWA KUWASILIANA MARA KWA MARA NA MCHUMBA WAKO? KWA SIMU AMA BARUA AMA E-MAIL?
 


JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.

Ama kuhusu kuwasiliana baina ya mvulana aliyeposa na posa yake kukubaliwa na msichana na walii wake basi hakuna tatizo lolote ikiwa mawasiliano yao ni katika mipaka ya kishariy'ah na mbele ya Mahaarim.

Wanachuoni wanaonelea mawasiliano baina ya wachumba kwa simu au kwa njia nyingine za faragha zozote zile hayaruhusiwi. Yote ni katika kuepusha fitnah na Shaytwaan kuingia baina yao kabla ya ndoa.

Mara nyingi mawasiliano ya karibu kabla ya ndoa, yameleta uharibifu mkubwa na madhara katika jamii na kusababisha posa nyingi kuharibika na hata watu kutumbukia katika zinaa.

Mbali na mawasiliano hayo mvulana anaweza kwenda nyumbani kwa mchumba wake bora tu wasikae faragha wao peke yao katika mazungumzo. Inabidi awe pamoja nao Mahaarim wa msichana. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakai faragha mwanamume na mwanamke ila wa tatu wao ni Shaytwaan. Na hakika Shaytwaan hutembea katika mwili wa mwana Aadam kama itembeavyo damu”.

Hii ni kuwa bado nyinyi hamjakuwa mume na mke, na mmoja kati yenu anaweza kuvunja ndoa hiyo baada ya kuwa mmekubaliana hapo awali. Mwanamume anaweza kusema basi hataki tena harusi au mwanamke vilevile kuamua kuwa hakuna tena harusi, na baya zaidi ni uwezekano wa kutokea maovu katika kipindi hicho.

Ile desturi ya wachumba kuwa wanakwenda pamoja katika mabustani, sinema au kusafiri kabla ya kuoana si desturi ya Kiislamu, japo kuna nchi nyingi za Waislamu wanafanya hivyo.
Asubiri Kumaliza Shule Kuolewa Au Aendelee Kuwa Na Mahusiano

Asubiri Kumaliza Shule Kuolewa Au Aendelee Kuwa Na Mahusiano


Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:

Asalaam alykum warahmatulahie wabarakatuh naomba Allaah swt awalipe malipo wazuri kuhusu kazi mnayoifanya awaweke katika pepo ya juu firdaus ameen Allaahuma ameen mimi. Nilikiwa ninaswahi. Mimi niko na mchumba na tunataka kuowana lakini bado myaka michache nimalize shule na haiwezekani tukafanya harusi kwa sasa lakini nafanya subra mpaka nimalize shule ndo tuowane je kwa hivi sio haram??


JIBU

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuolewa ukiwa katika masomo. Ndoa katika Uislamu ni maafikiano na ahadi ambazo wanachukua mume na mke katika njia ya halali. Ikiwa tayari umechumbiwa na mume na tayari mumeagana kuoana baada ya masomo inabidi wewe na yeye muepukane kabisa ili msije mkaingia katika madhambi.

Haifai Kiislamu watu walioposana kukutana faragha wala kuzungumza hata kwa simu ili lisije likatokea jambo ambalo halifai. Inabidi kila mmoja asubiri na aepukane na vishawishi vyote ambavyo vinaweza kuwakaribisha na zinaa. Ikiwa mnaona ya kwamba hamuwezi kuvumilia basi inabidi muoane ili muepukane na madhambi.

Tufahamu kuwa hakuna jambo lisilowezekana, wapo wasichana wengi walioolewa na wakaendelea na masomo bila matatizo. Ikiwa hamuwezi kusubiri na kujizuilia itabidi muoane na lau mtaweza kusubiri bila kuingia katika maasiya basi itabdi mfanye subira hadi mmalize malengo yenu ya masomo ndio muoane.

Tunamuomba Allaah Awape subira katika hilo, Aamiyn.

Sunday, May 12, 2019

Yuko Mbali Na Anayetaka Kumchumbia Je, Inafaa Kuongea Naye Kabla Ya Ndoa?

Yuko Mbali Na Anayetaka Kumchumbia Je, Inafaa Kuongea Naye Kabla Ya Ndoa?

Image result for NIKAAH  

Maswali: Posa-Sherehe
SWALI:

Assalamualeikum
Bismillahirrahmanirrahim


Alhamdulillah, mimi ni mwanamke wa miaka 21, nna kazi yangu na nipo masomoni kusomea hiyo kazi. Nina mchumba wangu hayupo hapa, yupo ulaya anatafuta maisha na ameshakuja kuleta wazee wake kwa wazee wangu lakini bado haijakubalika sababu wamesema wanataka miaka minne kwa ajili ya matayarisho ya kazi na kimaisha ya huyu mwanamme...jee inafaa mimi kua naongea nae? Na pia kupeana ushauri wa maisha yanavokwenda? Je inafaa? Wabillahi tawfiq




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuongea na mchumba wako ambaye amekataliwa na wazee wako. Mazungumzo baina ya mwanamme na mwanamke ni njia moja ya kukaribia zinaa, hiyo ni kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katujulisha kila kiungo cha mwanaadamu kinazini, mdomo ukiwa ndani ya tangazo hilo. Na Allaah Aliyetukuka Ametunasihi kuwa tusikaribie zinaa (al-Israa’ [17]: 32).

Na kulingana na swali lako wazee wako wamekataa posa mpaka baada ya miaka minne wakati ambao mchumba wako atakuwa amestakiri kimaisha. Kwa hiyo, wewe na yeye hamna hata hayo mahusiano ya uchumba. Kwa ajili hiyo, ni bora msiwe mkizungumza kungojea wakati atakapokuja tena na kuposa na kukubaliwa. Hata ikiwa amekubaliwa ni bora kuchukua tahadhari kubwa katika mazungumzo.


Kukubaliwa posa kwa mwanamme si kibali cha kuzungumza mnayotaka kwani hajakuwa mumeo. Kile kinachokubaliwa baada ya posa ikibidi ni yale mawasiliano ya muhimu yenye kuhusiana na masuala ya muhimu ambayo yasiyoingiliana na mapenzi na hisia ili Shaytwaan asiingie kati yenu.
Ndoa Ya Siri Inafaa Ikiwa Wazazi Hawataki?

Ndoa Ya Siri Inafaa Ikiwa Wazazi Hawataki?

Image result for NIKAAH

Maswali: Nikaah na Shariyah Zake 

SWALI:
Aslam Alyekum
Mie ni binti wa kiislam ambaye niko masomoni nchini Uingereza na nimepata mchumba muislam huku UK na anataka kunioa, lakini mtihani tulikuwa nao ni  kwamba mie nasomeshwa na wazazi wangu na kwamba wakijua kwamba ninamchumba na ninataka kuolewa nae watakataa kunilipa ADA ( School Fees). (Mchumba wangu hana uwezo wa kunilipia). 
Je naomba ushauri kama inawezekana binti kufunga ndoa kisiri bila wazazi wake kujua (au baba yake kumuodhesha ikiwa yuko hai?). Kusema ukweli huu ni mtihani mkubwa kwetu kwani uvumilivu wetu kila siku unapata mitihani na tunataka kufunga ndoa ili tufanye tendo lile kwa halali lakini kama nilivyosema wazazi wangu wakijua mie shule basi tena na bado nahitaji msaada wao kwa miaka miwili iliyobaki ya course yangu.
Naomba nijibiwe swali langu.


JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani nyingi kwa dada yetu aliyeuliza swali hili nyeti katika Dini na ambalo vijana wengi wanalipuuzia. Ifahamike kuwa ndoa katika Uislamu ina masharti yake au nguzo zake ambazo zinaifanya iwe halali na yenye kukubaliwa kisheria. Kukosekana nguzo mojawapo inaibatilisha ndoa hiyo. Nazo ni kama zifuatavyo 
1.    Kuwepo kwa walii ambaye ni baba, ikiwa hayuko au amekufa ndugu wa kiume, na kadhalika;
2.    Kwa uchache mashahidi wawili waadilifu;
3.    Namna ya kufunga ndoa: Ni Walii kumuozesha binti yake huyo mume na mume mwenyewe kukubali;
4.    Kutolewa mahari na mume.
Hakuna ndoa ya siri katika Uislamu, kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza kuwa ndoa itangazwe. Na ikiwa ndoa inayoitwa ya siri ni ile ambayo kwamba mume anaoa mke wa pili lakini hataki mkewe wa kwanza ajue hilo, basi itasihi ikiwa imetimiza masharti hayo hapo juu.

Mara nyingi huwa tunasema nimekutana na mvulana na namuona ameshika Dini, lakini mara nyingi huwa hatumjui vilivyo. Kwani utakuwa umekutana naye katika darasa na kupendana kwa kule kuonana tu mara ya kwanza. 

Kuwepo Walii katika ndoa ni kuhakikisha kuwa maslahi ya binti yametimizwa na kusiwe na udanganyifu wowote. Hii ni kuwa wasichana wanakuwa madhaifu na Uislamu unataka kuhakikisha kuwa maslahi yao na haki zao hazidhulumiki.
Katika kadhiya yako hii ni kuwa masharti ya ndoa hayajakamilika na kukaa pamoja au kuoana itakuwa mnazini na kupata madhambi. Kisha itakuwa taabu zaidi kwako lau mzazi atakuja kujua kuwa unakaa na mvulana nawe umemficha. Hiyo shida ambayo hutaki kuipata ndio itakuwa kubwa zaidi. Hakika ni kuwa huwezi kuliweka jambo hilo kuwa siri kwa muda wote wa miaka miwili ambayo upo chuoni. Unaweza kushika mimba au ikafika habari hiyo nyumbani. Utawajibu nini wazazi kuhusu hilo?

Nasiha zetu kwako za dhati ni kuwa mwanzo umfahamu zaidi huyo mume. Je, anazo sifa ambazo zinatakiwa mume wa Kiislamu awe nazo katika Dini, Ibadah, Maadili na mengineyo au umempenda kwa sababu ya sura zake na mengineyo. Miaka miwili si mingi na ikiwa huyo mvulana anakupenda kweli, basi anaweza kukusubiri mpaka umalize. Katika hali hiyo mnaweza mkawa mnafunga Swawm ya Sunnah ili kupunguza matamanio. Ni lazima msiwe mnakutana kama ilivyoagiza Dini ya Kiislamu ili msije mkafanya dhambi ambapo ndio mara nyingi hutokea. Ukiona huwezi vumilia basi itabidi uzungumze na mzazi wako ima mama au baba ambaye unaona anaweza kukuelewa kuhusu jambo hilo. Mara nyingi binti huwa anaweza kuzungumza kwa uwazi zaidi na mama ambaye naye anaweza kumueleza baba kuhusu hilo. Ikiwa wataelewa na kukufahamu basi itakuwa ni kheri lau wamekataa, basi jipinde katika masomo na InshaAllah tunamuomba Allah Aliyetukuka Akupatie lenye kheri nawe hapa duniani na kesho Akhera.
Usifanye haraka.
Na Allah Anajua zaidi

UMEZISOMA HIZI?

Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa